Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Idara ya Mahusiano ya Vyombo vya Habari ya Hizbullah imetangaza kwamba, baadhi ya watu mashuhuri na marafiki, kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, hutoa kauli, taarifa na habari mbalimbali, ambazo baadhi yake zinahusiana na masuala na matukio yanayohusiana na Hizbullah au Muqawama wa Kiislamu.
Idara hiyo ya Mahusiano ya Vyombo vya Habari imeeleza kwamba katika hali nyingi, umma huzipokea kauli na taarifa hizo kwa namna kana kwamba zimetolewa na vyanzo rasmi vya Hizbullah au Muqawama.
Mahusiano ya Umma ya Hizbullah yamesisitiza kwamba kila mtu ana haki ya kuchapisha taarifa yoyote kwa jina lake mwenyewe kupitia chombo au jukwaa lolote la habari, kwa sharti kwamba awajibike kwa taarifa hizo. Aidha, imewataka wananchi na umma kwa ujumla kuwa waangalifu katika kuzichukulia taarifa hizo kuwa ni taarifa rasmi.
Idara hiyo ya Mahusiano ya Vyombo vya Habari imefafanua kwamba; Hizbullah hutangaza misimamo yake kuhusu matukio na mabadiliko mbalimbali kupitia hotuba za Katibu Mkuu anayeheshimiwa, pamoja na taarifa rasmi zinazotolewa na Hizbullah, Muqawama wa Kiislamu, Idara ya Mahusiano ya Vyombo vya Habari, na Kundi la Wabunge wa Uaminifu kwa Muqawama. Imesisitiza kwamba chochote kinachotolewa nje ya njia hizo kinawakilisha maoni ya waliokitoa wenyewe.
Idara ya Mahusiano ya Vyombo vya Habari imehitimisha taarifa yake kwa kuwashukuru watu wote kwa uelewa na ushirikiano wao katika jambo hili, kwa lengo la kuzuia tafsiri yoyote isiyo sahihi au mkanganyiko, hususan katika kipindi hiki nyeti na muhimu.
Maoni yako